Huzuni na majonzi zilitanda katika kijiji cha Njoguini, kaunti ya Kirinyaga, katika mazishi ya Peter

  • | Citizen TV
    684 views

    Huzuni na majonzi zilitanda katika kijiji cha Njoguini, kaunti ya Kirinyaga, katika mazishi ya Peter Macharia, aliyeuawa wakati wa maandamano ya Saba Saba. Macharia, mwenye umri wa miaka 21, anaripotiwa kupigwa risasi na polisi akiwa anachuma majani chai karibu na kwao. Waliohudhuria mazishi hayo walishtumu serikali kwa kushindwa kuzuia mauaji ya vijana wakati wa maandamano.