Idadi ya vifo vya mafuriko yafikia 140

  • | Citizen TV
    506 views

    Zaidi ya watu 140 kufikia sasa wamerekodiwa kufariki kutokana na athari za mvua tangu wiki jana. Hii ni baada ya watu 93 kuripotiwa kufariki sehemu mbalimbali nchini kufikia jana jioni. Hii ni kabla ya vifo vilivyoripotiwa kuanzia leo asubuhi kutoka eneo la Mai Mahiu, Nakuru ambapo kufikia mwendo wa saa sita, watu 42 walikuwa wamefariki. Tana River, maiti moja ikiopolewa, Garissa mtu mmoja, Mathioya watu watatu wakifariki na Nyahururu mtu mmoja akifariki. Taarifa zaidi tutazipata kwenye taarifa zetu za baadaye