Idadi ya waliofariki Mwea Kirinyaga yafika watu 20

  • | Citizen TV
    1,081 views

    Idadi ya watu waliofariki baada ya kubugia pombe haramu huko Mwea Magharibi kaunti ya Kirinyaga imefikia watu ishirini hii leo. Mkasa huo umemchochea, Waziri wa usalama wa kitaifa profesa Kithure Kindiki kutangaza operesheni ya kukabiliana na pombe haramu na dawa za kulevya kote nchini mara moja .