Idara ya anga yasema mvua nyingi kupungua maeneo mengi

  • | Citizen TV
    2,294 views

    Idara ya utabiri wa hali ya anga nchini sasa imetangaza kuwa mvua kubwa inayoshuhudiwa sehemu nyingi nchini itapungua kufikia mwanzo wa mwezi mei. Kwa mujibu wa idara hii, Mvua nyingi sasa inatarajiwa zaidi maeneo ya Pwani na magharibi ya Kenya ambayo hayajashuhudia mvua kwa wingi katika siku za punde. Mkurugenzi wa idara hii Dakta David Gikungu akisema nyanda za juu za mashariki mwa bonde la ufa na Nairobi bado kutaendelea kushuhudia mvua japo kwa kiwango cha chini