Idara ya misitu nchini yatoa onyo kwa wakazi wanaochoma makaa Garissa

  • | Citizen TV
    292 views

    Idara ya misitu nchini - KFS Imetoa onyo kwa wakaazi wa kaunti ya Garissa wanaojishughulisha na uchomaji makaa kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Kamanda wa misitu kaunti ya Garissa Naseeb Mwamusi amesema idara yake itaendelea kushika doria katika maeneo ambapo biashara ya makaa Inaoneka kunoga. Akizungumza baada ya upanzi wa miche zaidi ya mia moja kusherehekea miaka 20 tangu kubuniwa kwa mamlaka ya kusimamia mazingira -NEMA, mkurugenzi wa mamlaka hiyo Issac Kimitei aliwarai wenyeji kupanda miti wakati huu wa mvua ya vuli ili kukabiliana na changamoto za tabianchi