IEBC almaarufu Cherera four leo wanadai kuwa walipokea vitisho nakulazimishwa kujiuzulu.

  • | KBC Video
    37 views

    Waliokuwa makamishna wa tume ya IEBC almaarufu Cherera four leo wameiambia kamati ya kitaifa ya mazungumzo kuwa walilazimishwa kujiuzulu. Aidha, wamedai kuwa walipokea vitisho ,suala lililowafanya Juliana Cherera na Irene Massit kuondoka humu nchini. Hata hivyo, hawafafanua zaidi kuhusu vitisho hivyo wala kueleza vilitolewa na nani na ni kwa nini hawakuripoti kisa hicho kwa maafisa wa polisi. Na kama vile mwanahabari wetu Giverson Maina anatuarifu, wanne hao walipendekeza kubuniwe jopo la kushughulikia mizozo iwapo makamishna wa tume hiyo watakosa kukubaliana katika siku za usoni.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News