- 156 viewsTume ya uchaguzi na mipaka IEBC imelalamikia idadi ndogo ya vijana wanaojitokeza kujisajili kuwa wapiga kura. Tume hiyo kufikia sasa ikiwasajili wapiga kura 148,000 tu kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita. Hata hivyo, leo jukwaa la kuchukua maoni kutoka kwa wadau wa uchaguzi mdogo uliopita, liligeuka ukumbi wa majibizano kati ya makamishna wa IEBC na baadhi ya vijana waliohudhuria kikao hicho