Tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka IEBC, inataka bunge kuongeza muda wa kutatua kesi za kisiasa ambao kwa sasa ni siku kumi. wakizindua ripoti ya suluhu za kesi za kisiasa hapa jijini nairobi, makamishna wa IEBC wanasema huenda migogoro ikaongezeka katika uchaguzi mkuu ujao kwa sababu ya ongezeko la vyama vya kisiasa. Mwenyekiti wa tume hiyo Erastus Ethekon anasema wamesikitishwa na fujo za Ol kalou wakiwataka washirika wote wa uchaguzi mdogo wa ubunge utakaofanyika alhamisi wiki ijayo kuzingatia sheria .