Ikulu ya rais yakosa kuthibitisha kuhusu ziara ya Rais Suluhu

  • | Citizen TV
    11,007 views

    Jioni ya leo, Ikulu ya Rais imeshikilia kuwa haikuwa na ufahamu kuhusu ziara ya rais Samia Suluhu wa Tanzania endapo alikuwa hapa nchini Kenya. Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed akisema hakukuwa na mipango ya itifaki iliyofanywa na serikali, kwenye taarifa iliyodinda kuthibitisha au kukana kuwa rais huyo wa Tanzania alikuwa nchini kutafuta mwafaka kati ya Rais William Ruto na Raila Odinga.