Imesalia siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa Marekani

  • | Citizen TV
    3,841 views

    Ikiwa imebaki siku moja kabla ya uchaguzi mkuu wa Marekani hapo kesho Jumanne, wasi wasi umetanda nchini humo kutokana na kwamba uchunguzi wa taasisi za maoni unaonesha hakuna mshindi wa moja kwa moja kati ya Kamala Harris na Donald Trump. Kilicho wazi ni kwamba watu wanaonekana kuwa na ari ya kushiriki katika uchaguzi kutokana na idadi ya waliopiga kura zao tayari imefikia milioni 71 ikiwa idadi kubwa kuwahi kutokea.