Inspekta Jenerali Japheth Koome asema polisi hawakuvunja sheria wakati wa maandamano

  • | Citizen TV
    1,122 views

    Inspekta Jenerali Japheth Koome amedai kuwa upinzani unaendesha propaganda dhidi ya polisi, akidai kuwa umekuwa ukionyesha maiti za watu waliokufa kwa njia tofauti na kudai kwamba waliuwawa na polisi wakati wa maandamano. Akiongea na wanahabari katika chuo cha mafunzo ya polisi huko kiganjo kaunti ya Nyeri, Koome amewatetea polisi akisema hawakuvunja sheria yeyote walipokuwa wakikabiliana na waandamaji.