Inspekta wa polisi Ahmed Rashid aagizwa kujisalimisha katika afisi ya mkuu wa DCI mjini Garissa

  • | K24 Video
    264 views

    Mahakama ya Milimani imeairisha kesi ya afisa wa polisi Ahmed Rashid aliyetarajiwa mahakamani kujibu mashtaka anayokabiliwa nayo ya mauaji hadi tarehe 9 februari mwaka huu. Rashid anahusishwa na mauaji ya wanaume wawili yaliyotokea mtaani eastleigh mnamo machi mwaka wa 2017 baada ya uchunguzi wa mamlaka ya IPOA. Rashid ametakiwa kushirikiana na polisi ili kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kabla ya kushtakiwa tarehe hiyo iliyopangwa.