Israel yaendeleza vita dhidi ya Hamas na Islamic Jihad
Jeshi la Israeli limetoa kanda ya video Jumatano (Julai 10) ikionyesha kile walichosema ni majeshi ya ardhini yakifanya operesheni Gaza wakati mashauriano ya kusitisha mapigano katika vita vilivyodumu kwa miezi tisa yamepangwa kuanza tena.
Jeshi la Israeli lilisema katika taarifa yake kuwa majeshi yake yalikuwa yanaendelea na operesheni huko Gaza City dhidi ya wanamgambo wa Hamas na washirika wao Islamic Jihad, ambao walisema walikuwa wanafanya mashambulizi kutoka katika kituo cha UNRWA, wakikitumia kama ni ngome yao ya kufanya mashambulizi.
Kulingana na jeshi la Israeli walikuwa wamefanyia operesheni zao katikati mwa Gaza na Shejaiya.
Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha eneo linaloonyeshwa katika kanda ya video. Reuters imeshindwa kupata uthibitisho huru wa tarehe ambayo video hiyo ilichukuliwa.
Vita hiyo ilianza Oktoba 7 wakati wapiganaji kutoka Palestina wa kikundi cha wanamgambo wa Hamas walipovamia mpakani na kushambulia jamii mbalimbali huko Israel, ikiuwa watu 1,200 na kuwateka watu 250, kulingana na idadi iliyotolewa na Israeli.
Shambulizi la Israeli huko Gaza kulipiza kisasi lilianza siku hiyo hiyo kwa kushambulia kwa mabomu na limeendelea kwa miezi tisa pamoja na uvamizi wa ardhini ambapo mamlaka za afya Palestina zinasema imeuwa zaidi ya watu 38,000 na kujeruhi zaidi ya watu 80,000.
Idadi kubwa ya waliojeruhiwa kutokana na vita hivyo imeongeza magonjwa kusambaa na utapiamlo kati ya wakazi asilimia 90 wa Gaza ambapo Umoja wa Mataifa unasema wamekoseshwa makazi, na kuweka shinikizo kubwa kwa mifumo ya afya katika eneo hilo finyu. - Reuters
#Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi #wahouthi #marekani #uingereza #shambulizi #dhamar #yemen #hospitali #nasserhospital
11 Aug 2025
- Over the last week, three MSS officers lost their lives.
10 Aug 2025
- Kenyans have been urged to report hospitals charging for certain SHA services.
10 Aug 2025
- The chief officer for environment will seek reinforcement from thousands of workers.
11 Aug 2025
- Shortly after the strike, the IDF confirmed that it had targeted Anas al-Sharif, who "served as the head of a terrorist cell in Hamas".
11 Aug 2025
- The video widely shared on TikTok claims that the ’23-year-old’ was attacked during a performance.
11 Aug 2025
- Among those killed was the bride-to-be, Jackline Kasau, 42.
11 Aug 2025
- Over the last week, three MSS officers lost their lives.
11 Aug 2025
- Why Nairobi Hospital is in battle for survival
11 Aug 2025
- 28 years in bed: Naomi's relentless fight for dignity
11 Aug 2025
- Devolution system's good, bad and ugly 12 years later
11 Aug 2025
- Like Jomo Kenyatta and Kwame Nkrumah, 'saviour' Ruto has disappointed
11 Aug 2025
- Gachagua, Ruto and Uhuru face crucial Mt Kenya by-election test
11 Aug 2025
- Wild cheers, wild bites: Football meets game meat in Dar es Salaam