Itachukua muda kubaini kilichosababisha kifo cha Rita Waeni, asema mwanapatholojia mkuu wa serikali

  • | KBC Video
    118 views

    Itabidi Wakenya wavute subira kabla ya kupata taarifa kamili kuhusu kilichosababisha kifo cha Rita Waeni, mwanafunzi wa umri wa miaka 20 ambaye mwili wake ulikatwakatwa katika chumba kimoja cha malazi mtaa wa Roysambu kaunti ya Nairobi. Baada ya uchunguzi wa mwili huo, mwanapatholojia wa serikali Johansen Oduor alisema mwili wa Rita ulikatwakatwa kwa msumeno, japo hakujaribu kujinasua. Kwa mujibu wa Oduor, tukio hilo ni nadra sana na wanapatholojia wenzake wamechukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi wa kina katika maabara ya serikali.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive