Jaji Daniel Ogembo apatikana amefariki nyumbani kwake

  • | KBC Video
    36 views

    Jaji msimamizi wa mahakama kuu ya Siaya Daniel Ogola Ogembo alipatikana amefariki leo asubuhi nyumbani kwake mjini Siaya.Kulingana na polisi,mwili wa marehemu ulipatikana dereva wake alipokwenda kumchukua kumpeleka kazini .Hadi sasa kilichosababisha kifo chake hakijabainishwa. Marehemu jaji Ogembo yasemekana alikuwa kazini jana akiwa buheri wa afya.Mwili wa marehemu sasa unasubiriwa kufanyiwa upasuaji kubaini kilichosababisha kifo chake.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive