Jaji Mkuu Koome akosoa utendakazi wa mkandarasi wa ujenzi wa mahakama Mombasa

  • | KBC Video
    36 views

    Jaji mkuu Martha Koome amesikitishwa na kile amekitaja kuwa utendakazi mbovu wa mwanakandarasi aliyepewa jukumu la ujenzi wa jengo la kisasa la mahakama mjini Mombasa la thamani ya mamilioni ya pesa Koome alisikitika kwamba fedha zilizolipwa mwanakandarasi huyo ni kama zilizopotea baada ya ripoti za uchunguzi wa tume ya huduma ya mahakama kutathmini hali ya jengo hilo linalokadiriwa kugharimu shilingi milioni 445. Jengo hilo la ghorofa nne limejengwa kwenye kipande cha ardhi chenye ukubwa wa ekari 3.6 mkabala wa majengo ya awali ya mahakama yaliyojengwa mnamo mwaka 1984.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channell: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #marthakoome #darubini