Jaji Mkuu Martha Koome awataka polisi kuwajibika kwenye maandamano

  • | Citizen TV
    2,671 views

    Jaji mkuu Martha Koome amewataka maafisa wa polisi kutofautisha waandamanaji wa amani na majangili wanaozua vurugu, kuiba na kuharibu mali wanapowakamata waandamanaji na kuwafikisha kortini. Koome ameelezea masikitiko yake kuhusiana na polisi kutumia nguvu kupita kiasi. Haya yanajiri huku Naibu Rais Prof. Kithure kindiki akisema hali ya ukosefu wa ajira kati ya vijana imechochea pakubwa maandamano ambayo yameshuhudiwa nchini katika siku za hivi punde.