Jamaa aliyetekwa nyara arejea nyumbani akiwa buheri wa afya

  • | Citizen TV
    2,241 views

    Ni furaha tele kwa familia moja katika eneo la Witeithie, kaunti ya Kiambu baada ya jamaa yao aliyetoweka baada ya kutekwa nyara wakati wa maandamano dhidi ya serikali kupatikana akiwa salama. Joseph Mwangi mwenye umri wa miaka 28, anaripotiwa kutekwa nyara katika eneo la Githurai mnamo juni 18 na kusafirishwa hadi eneo lisilojulikana kisha kuachiliwa baadaye.