James Kariuki, Simeon Omondi na David Kitavi washinda 'Taste Off'

  • | Citizen TV
    534 views

    James Kariuki, Simeon Omondi na David Kitavi ndio washindi wa mashindano wa kupika ya kipindi cha taste off kilichokuwa kikipeperushwa kwenye runinga ya citizen kila Jumamosi usiku. Ilikuwa ni furaha na mbwembwe kwa washindi hawa waliojumuika na familia zao. Watatu hawa waliibuka kidedea kati ya wawaniaji 16 waliofuzu baada ya mchujo mkali kutoka kwa wawaniaji mia nne. Washindi hao walipata tuzo tofauti huku James Kariuki akishinda tuzo ya shilingi millioni moja. Kipindi cha taste off kimekuwa kikipeperushwa hapa citizen tv tangu mwezi Mei.