Jamii inayoteka maji makaburini nchini Zimbabwe

  • | BBC Swahili
    Wakazi wa Hopley kusini mwa Harare, Zimbabwe wamechukua hatua ya dharura kujihakikishia upatikanaji wa maji. Baada ya maji ya visima kukauka, watu wamelazimika kutumia kisima kilichopo karibu na eneo la makaburi. Kuna hofu maji hayo huenda yamechanganyika na uchafu kutoka kwa miili ya watu waliozikwa hapo. Lakini wataalamu wanasema mvua ikinyesha huenda ikapunguza hatari hiyo kwa 20%, kwa sasa vyanzo kama hivi vya maji huenda ndio njia pekee ya kijipatia bidhaa hii muhimu. #bbcswahili #Zimbabwe #miundombinu