Jamii wa Talai inayoishi sehemu mbalimbali nchini Kenya imewasilisha maombi ya kutambuliwa kwa kitengo cha kuzingatia maslahi ya walio wachache na waliotengwa kutoka ofisi ya rais.
Katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Kiprugut Chumo uliowaleta pamoja wanajamii wa Talai kutoka Kaunti ya Kericho, Meru, Baringo, Mandera, Homabay, Narok na Bomet wakiongozwa na Katibu wao Lowoi wanataka serikali kuzingatia haki yao kutokana dhulma za kikoloni, na kutambuliwa Kama jamii tofauti na iliyoko na kanuni zake.