Jamii ya Wasomali huko Isiolo imewasilisha malalamishi kwa NLC

  • | Citizen TV
    Wasomali kutoka koo za Isaak na Harti wamewasilisha malalamishi yao kwa tume ya kitaifa ya ardhi NLC kabla ya muda uliowekwa kwa shughuli hiyo kukamilika. Wakiongozwa na mwenyekiti wa baraza la wazee Said Ali Salad, waakilishi wa jamii hiyo waliwasilisha stakabadhi zenye malalamishi yao kuhusu ukiukaji wa haki zao kwa mshirikishi wa tume hiyo eneo la Isiolo Paul Kasimbu.