Jamii ya Waturkana yampongeza rais kwa kumteua Ethekon kuwa mwenyekiti wa IEBC

  • | Citizen TV
    1,004 views

    Kuteuliwa kwa wakili Erastus Edung Ethekon kuwa mwenyekiti mpya wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kutoka jamii ya Waturkana, kumewafurahisha sana wakazi wengi wa Turkana wakisema uteuzi huo ni wa kipekee na kihistoria. Mwanahabari wetu Cheboit Emmanuel amezuru nyumbani kwake na ofisi alikokuwa akifanyia kazi kabla kuteuliwa na kutuandalia ripoti yake kutoka Lodwar.