- 178 viewsWatu 157 wamefariki Jumatatu katika maporomoko ya ardhi katika eneo la mbali la Kusini mwa Ethiopia, maafisa wa eneo hilo wamesema, wakionya kwamba idadi ya vifo inaweza kuongezeka. “Zaidi ya miili 55 ilipatikana kutokana na maporomoko hayo, taarifa kutoka idara ya masuala ya mawasiliano ya eneo la Gofa ilisema, ikimnuku kiongozi wa eneo hilo Dagmawi Zerihun, ambaye alionya kuwa idadi ya “vifo bado inaweza kuongezeka”. Maporomoko hayo yalitokea saa nne asubuhi majira ya huko kufuatia mvua kubwa katika eneo lenye milima la jimbo la kusini mwa Ethiopia, Dagmawi alisema. Wanawake na watoto ni miongoni mwa waliofariki, alisema, akiongeza kuwa shughuli za kuwatafuta manusura “zimekuwa zikiendelea”. Picha zilizosambazwa kwenye mtandao wa Facebook na chombo cha habari kinachoshirikiana na serikali, Fana Broadcasting Corporate zilionyesha mamia ya watu karibu na eneo la tukio lililoharibika lenye udongo mwekundu ulioporomoka. Eneo la Gofa lipo umbali wa kilomita 450 kutoka mji mkuu Addis Ababa, mwendo wa masaa 10 kwa kutumia gari. Jimbo hilo la kusini mwa Ethiopia limeathiriwa na mvua za muda mfupi za msimu kati ya mwezi Aprili na mapema mwezi Mei ambazo zimesababisha mafuriko na watu wengi kuhama makazi yao, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kutoa misaada ya dharura ya kibinadamu (OCHA). - AFP #voa #voaswahili #ethiopia #janga #maporomoko #matope #vifo #uokoaji
Janga la Maporomoko ya Matope Yaua Watu 157
- 13 May 2025 - The Employment and Labour Relations Court in Kakamega has given a green light to a case filed by 17 doctors citing their unpaid salaries and alleged unfair dismissals by the county government.
- 13 May 2025 - The Moi Teaching and Referral Hospital (MTRH) has successfully performed its first Stereotactic Radiosurgery (SRS) procedure.
- 13 May 2025 - Operations at Belgium's second largest airport were suspended on Tuesday due to a bomb alert on an aeroplane, the company running the airport said.
- 13 May 2025 - The Persons with Disabilities Bill, 2025, is set to offer people with disabilities tax exemptions and reliefs that will significantly improve their quality of life and enhance their access to services.
- 13 May 2025 - Deputy President Kithure Kindiki has dismissed opposition leaders inciting public dissent against the Kenya Kwanza administration.
- 13 May 2025 - The route is expected to ease traffic on the Nairobi-Mai Mahiu route.
- 13 May 2025 - The MP gave several reasons as to why he wants the military to be deployed.
- 13 May 2025 - Kenyans raised concerns about possibly being subjected to higher interest rates.
- 13 May 2025 - The fertiliser was found in some incidents to contain sand and stones, sparking public uproar.
- 13 May 2025 - Healthcare workers under the Universal Health Coverage (UHC) program countrywide on Monday demonstrated outside the Ministry of Health headquarters at Afya House in Nairobi.