Je mtu yeyote anaweza kuwa rais wa Marekani?

  • | VOA Swahili
    46 views
    Hapana. Kazi iko wazi kwa wale wana sifa zilizotajwa katika Katiba ya Marekani. Mahitaji: Awe na Umri wa miaka 35 Awe ameishi ndani ya Marekani kwa miaka 14. Awe raia mzaliwa wa Marekani. Wasisi wa taifa walikuwa na matumaini umri huenda ukaleta busara na ukomavu. Wakati Katiba ilipokuwa inapitishwa umri wa kuishi ulikuwa chini ya miaka 40 Ukazi na uraia: Mahitaji haya yalikuwa na azma ya kukatisha ushawishi wa nje. Wataalamu wa kisheria wanaamini uraia wa kuzaliwa unahusu mtu aliyezaliwa nchini Marekani au aliyezaliwa na wazazi ambao ni Wamarekani. Lakini Mahakama ya Juu Marekani haijawahi kutoa maamuzi rasmi kuhusu ufafanuzi wa suala hili. #uchaguzi #marekani #upigajikura #mhamiaji #greencard #raia #ukaaziwakudumu #voa #voaswahili #sifa #kugombea #nafasiyaurais #sifa #wazazi #kuzaliwa