Je mtu yeyote anaweza kuwa rais wa Marekani?⁣⁣

  • | VOA Swahili
    44 views
    Hapana. Kazi iko wazi kwa wale wana sifa zilizotajwa katika Katiba ya Marekani.⁣ Mahitaji:⁣ Awe na Umri wa miaka 35⁣ Awe ameishi ndani ya Marekani kwa miaka 14.⁣ Awe raia mzaliwa wa Marekani.⁣ Wasisi wa taifa walikuwa na matumaini umri huenda ukaleta busara na ukomavu.⁣ Wakati Katiba ilipokuwa inapitishwa umri wa kuishi ulikuwa chini ya miaka 40⁣ Ukazi na uraia:⁣ Mahitaji haya yalikuwa na azma ya kukatisha ushawishi wa nje.⁣ Wataalamu wa kisheria wanaamini uraia wa kuzaliwa unahusu mtu aliyezaliwa nchini Marekani au aliyezaliwa na wazazi ambao ni Wamarekani.⁣ Lakini Mahakama ya Juu Marekani haijawahi kutoa maamuzi rasmi kuhusu ufafanuzi wa suala hili.⁣ ⁣ #uchaguzi #marekani #upigajikura #mhamiaji #greencard #raia #ukaaziwakudumu #voa #voaswahili #sifa #kugombea #nafasiyaurais #sifa #wazazi #kuzaliwa