Je, ni sahihi, kuitumia sheria ya ugaidi dhidi ya waandamanaji?

  • | BBC Swahili
    3,165 views
    Katika wiki za hivi karibuni, taifa la Kenya limekumbwa na msuguano mkubwa kati ya wananchi na serikali kufuatia maandamano yaliyoshuhudiwa katika sehemu mbalimbali za nchi. Kinachozua mjadala mkubwa sasa ni hatua ya serikali kuwashtaki baadhi ya waandamanaji, wakiwemo wabunge na wanaharakati kwa makosa ya ugaidi. Hata hivyo, wakosoaji wanasema sheria hiyo sasa inatumika kama silaha ya kisiasa ya kuwanyamazisha wakosoaji na kuzuia maandamano halali. Mwandishi wa BBC Laillah Mohammed ametuandalia Habari hii. 🎥: @frankmavura #bbcswahili #kenya #maandamano Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw