"Je nini kimewapata wezi wa watoto Nairobi?"

  • | BBC Swahili
    526 views
    Baada ya miaka mitatu kupita, BBC Africa Eye inatembelea tena baadhi ya vitongoji maskini zaidi vya Nairobi ili kujua vita dhidi ya ulanguzi wa watoto nchini Kenya imefikia wapi kufuatia uchunguzi wa 2020 kuhusu mtandao wa 'Wezi wa Watoto'. Mnamo 2020 BBC Africa Eye ilifichua mtandao wa walanguzi wa watoto nchini Kenya, ambapo maofisa walitoa ahadi ya kuchukua hatua. Je, haki imetendeka? Na mambo yamebadilika kiasi gani tangu wakati huo? #bbcswahili #BBCAfricaEye #weziwatoto Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw