Je raia wanaweza kulinda kura mara baada ya kupigaji kura?- Dira ya Dunia Ijumaa 16th Oktoba

  • | BBC Swahili
    Tulionayo katika Dira ya Dunia Ijumaa 16th Oktoba · Baada ya mgombea Urais wa Zanzibar, kupitia chama cha ACT Wazalendo kufungiwa na Tume ya Taifa ya uchaguzi kufanya Kampeni, Maalim Seif asema hajui kosa lake. · Leo ni siku ya chakula duniani huku mabadiliko ya tabia nchi, ni kati ya sababu zilizotajwa kusababisha upungufu wa uzalishaji wa chakula katika mataifa mengi duniani · Wagombea wawili wa nafasi ya urais nchini Marekani wametoa tathmini zao za jinsi nchi hiyo inavyoshughulikia mgogoro wa Virusi vya corona · Ofisi kuu ya takwimu nchini Kenya imedokeza kuwa uchumi wa nchi hiyo umezorota kwa kiwango kikubwa kutokana na makali ya janga la Covid 19. · Na katika mjadala hii leo tunauliza, Je raia wanaweza kulinda kura mara baada ya shughuli ya upigaji kura? Tuwe pamoja ifikapo hapo kumi na mbili unusu jioni , mimi ni Regina Mziwanda na mwenzangu ni Lynace Mwashighadi #DirayaDunia #MaalimseifShariff #UchaguziTanzania2020