Je unaifahamu AL- Kasus?

  • | BBC Swahili
    Katika mfululizo wa chakula cha mtaani eneo la Afrika mashariki leo hii tunaangazia kinywaji maarufu kama AL- Kasus, kinywaji hiki inasemeka kimeziolea umaarufu wake katika maeneo ya pwani, kuanzia Tanga, Zanzibar na Dar es salaam nchini Tanzania. Kinywaji hiki ni mchanganyiko wa unga wa miti, viungo na mbegu kisha kuchangwa na maziwa au kunywewa kavu bila maziwa. Lakini kwanini kinywaji hiki kinapendwa sana hasa na wanaume? Angalizo :Taarifa hii si ushauri wa kitaalamu, kama una matatizo ya kiafya tafadhali waone wataalamu wa afya.