- 12,579 viewsDuration: 2:33Wataalamu wa afya kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Tanzania, wanasema kuwa vijana wengi hugundulika kuwa na magonjwa ya figo wakiwa tayari katika hatua za juu za ugonjwa, kutokana na kutofanya uchunguzi wa afya mara kwa mara. Wanasema ongezeko la vijana walio chini ya umri wa miaka 50 wanaoathiriwa na magonjwa ya figo linahusishwa zaidi na mabadiliko ya mtindo wa maisha pamoja na kuchelewa kugundua ugonjwa katika hatua za awali. Tarsila Emmanuel Chuleha ni Muuguzi Bingwa wa Magonjwa ya Figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kitengo cha Kusafisha Damu (Dialysis), amezungumza na @martha_saranga #bbcswahili #tanzania #afya Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw