Je, utasali vipi sala ya Eid ul Fitr ukiwa nyumbani?

  • | BBC Swahili
    Huku mwezi mtukufu wa #Ramadan ukielekea kufika mwisho. Lakini wakati huu mambo ni tofauti kwasababu ya janga la virusi vya corona. Hivyo basi, nchi mbalimbali zimechukua hatua ili kuhakikisha virusi hivyo vinadhibitiwa miongoni mwayo ikiwa ni kutokaribiana, kunawa mikono mara kwa mara na kadhalika. Lakini pia kwa wengi swala ya sikukuu ya Eid ul-Fitr haitakuwa kama kawaida. Mfano nchini Kenya ni wazi kwamba waumini wa dini ya Kiislamu wanahitajika kusali sala hii nyumbani. Sasa je sala ya Eid al-Fitr inaswaliwa vipi nyumbani? Fuatilia maelezo ya Sheikh @hassan.kinyua #eid #eidmubarak #ramadan #ramadan2020 #kenya🇰🇪 #tanzania #rwanda #uganda