Jenerali Francis Ogolla alisifiwa kwa bidii yake kazini

  • | Citizen TV
    1,046 views

    Familia ya jenerali Francis Ogola imemtaja kama mkristo shupavu, kaka mwaminifu na rafiki ambaye upendo wake kwa mungu haulinganishwi na wengi. ndugu zake walizua uchesi kwa umati walipoelezea jinsi marehemu ogolla aliishi maisha yake kwa usahihi na pia kupanga mazishi yake kwa usahihi huo huo, huku akilitaka jeshi kumlipia mkewe likizo baada ya mazishi. mwanawe joel Rabuku alielezea jinsi baba yake alikuwa na shauku ya kuinua na kuisaidia jamii yake, na aliahidi kuendeleza kazi aliyoianzisha babake.