Jengo jipya la bunge lazinduliwa

  • | KBC Video
    47 views

    Rais William Ruto ametoa changamoto kwa wabunge kutumia ipasavyo jengo la kisasa la Bunge Towers kutoa huduma bora kwa wananchi. Akizungumza hii leo alipofungua rasmi jumba hilo lenye vifaa vya kisasa, Rais Ruto alisema raslimali nyingi zilizotumiwa kwa ujenzi wa jengo hilo zinafaa kuongeza maradufu juhudi za wabunge katika mijadala, uwakilishi, na utungaji sheria kwa manufaa ya wakenya. Jengo hilo ambalo lina afisi 331 za wabunge, afisi za wasimamizi wa bunge na vyumba 26 vya mikutano ya kamati za bunge linatazamiwa kutoa mazingira bora kuwaruhusu wabunge kutekeleza wajibu wao ipasavyo.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive