Jeshi la Israel lagundua shimo la handaki la Hamas katika eneo la hospitali ya Al Shifa.

  • | VOA Swahili
    610 views
    Jeshi la Israel lilisema Alhamisi (Novemba 16) kwamba liligundua shimo la handaki la Hamas na gari lenye silaha katika eneo la hospitali ya Al Shifa huko Gaza. Wanajeshi pia walitoa video kwa umma na picha za handaki zikiwa na silaha. Reuters iliweza kuthibitisha eneo la video kwenye muundo wa majengo na ambazo ziliambatana na picha za eneo hilo. Hata hivyo Reuters haikuweza kuthibitisha tarehe ambayo video ilichukuliwa.