Jeshi la Israel lajiandaa na uvamizi wa ardhini Rafah

  • | VOA Swahili
    173 views
    Jeshi la Israel limesema leo linapeleka vitengo viwili vya vikosi vya akiba katika Ukanda wa Gaza. Hatua hiyo imechukuliwa wakati inajiandaa na uvamizi wa ardhini katika mji wa kusini mwa Rafah. Jeshi limesema vikosi hivyo vitafanya operesheni za ulinzi na mbinu lakini halikutoa maelezo zaidi kuhusu mpango wenyewe. Vita kati ya Israel na Hamas vilianza baada ya shambulizi la Oktoba 7, ambapo Hamas walivishitukiza vikosi vya ulinzi mbalimbali vya Israel na kuvamia jamii kadhaa, wanamgambo hao wa Palestina waliwauwa watu 1,200, wengi wao raia.⁣ ⁣⁣⁣ #Haifa ⁣⁣⁣⁣⁣#waelaldahdouh #hamzaaldahdouh #shirikalamwezimwekundu⁣⁣⁣ #Rafah #Netanyahu #Misri #Hamas #Gaza #Palestina #IDF #GalMeirEizenkot #mauaji #jeshi #israel #voa #voaswahili #mwandishi #aljazeera #maghazi