Jeshi la Israel yatoa video ya wanamgambo wa Hamas wakiwapeleka Mateka hospitali

  • | VOA Swahili
    345 views
    Jeshi la Israel siku ya Jumapili (Novemba 19) lilitoa kanda ya video iliyoonyesha picha ya kile walichosema walikuwa wanamgambo wa Kiislamu wa Hamas wakiwapeleka mateka kutoka Israel na kuingia katika Hospitali ya Shifa siku hiyo ya shambulizi la Oktoba 7. Video ilionyeshwa na msemaji mkuu Admirali Daniel Hagari ambaye alionekana kulionyesha kundi la wanaume wakiendeshwa kichura kuingia katika hospitali, na kuwashangaza wafanyakazi wa afya. Kanda ya pili ilimuonyesha mwanamme aliyejeruhiwa akiwa katika machela. Mwanamme mwingine aliyekwua karibu, akiwa na nguo za kiraia, na bunduki ya kivita.