Jeshi la wanahewa laadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa

  • | Citizen TV
    1,200 views

    Rais William Ruto ametoa ahadi kwa wanajeshi wa angani kuwa serikali itahakikisha imefadhili mafunzo ya marubani 200 kila mwaka. Rais Ruto aliyehudhuria hafla ya kusherehekea miaka 60 tangu kuanzishwa kwa kikosi cha wanajeshi wa angani pia ameongeza kuwa serikali itawekeza katika vifaa vya kisasa vya kulinda anga ya taifa. Katika hafla hiyo aliyekuwa kamanda wa kwanza mwafrika wa kikosi hicho Dedan Gichuru na marehemu Jenerali Francis Ogolla walituzwa kwa ueledi wao wa kuongoza kikosi.