Jinamizi barabarani I Watu-15 waangamia katika saa-24 zilizopita

  • | KBC Video
    86 views

    Watu-15 walipoteza maisha yao katika ajali tofauti za barabarani katika muda wa saa 24 zilizopita. Watu saba walifariki huku wengine kadhaa wakipata majeraha jana usiku baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana ana kwa ana na gari lingine katika kaunti ya Kericho. Kwingineko, watu wanane walifariki katika ajali ya barabarani iliyohusisha gari la uchukuzi wa umma na lori karibu na daraja la Ngata kwenye barabara kuu ya Nakuru-Eldoret. Hayo yanajiri huku halmashauri ya kitaifa ya uchukuzi na usalama barabarani ikitoa wito kwa madereva kuwa waangalifu wakati huu wa msimu wa mvua ambao hughubikwa na hatari nyingi.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1tv Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #Kenya #News