Jinsi wajasiriamali wanawake wanavyochangia kuhifadhi mazingira

  • | VOA Swahili
    92 views
    Wanawake wawili wajasirimali nchini Msumbiji wameanzisha biashara ambayo itasaidia kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa na kupunguza uchafu wa mazingira, Amarilis Gule anaripoti kutoka katika mji mkuu, Maputo. Vania Lazaro hupenda kuongeza mmea mpya katika bustani yake kila inapowezekana. Zaidi ya miezi sita iliyopita, amekuwa akijaribu kufanya majaribio ya mbolea mpya katika bustani yake ya maua na mboga nyumbani kwake Maputo, Msumbiji. Anasema anaishukuru bidhaa hiyo — inayoitwa N'toko Organic — mimea yake ina afya... Dima Jone si mwanamke pekee anayeendesha biashara ya mbolea ya asili nchini Msumbiji. Takriban miaka mitano iliyopita, Karina Jamal alianzisha Koko Boxes, biashara ambayo ilikuwa ikisambaza mbolea ya asili na upakiaji na mifuko ya mazingira rafiki. Jamal amesema anataka kuanzisha biashara thabiti wakati akiwahamasisha wanawake wengine. #wanawake #wajasiriamali #msumbiji #biashara #haliyahewa #uchafu #mazingira #amarilisgule #karinajamal