JSC yatafuta msajili wa mahakama

  • | Citizen TV
    453 views

    Tume ya huduma za mahakama nchini JSC imeanza mahojiano ya kujaza nafasi ya Msajili wa mahakama baada ya Anne Amadi kustaafu mwezi Januari. JSC imewaorodhesha watu 43 kujaza nafasi hii. Wanaohojiwa leo ni pamoja na;Macharia Rose Wachuka anayehudumu kama mkuu wa wafanyakazi katika ofisi ya Jaji Mkuu Martha Koome, Ouma Jack Busalile, Mokaya Frida Boyani, Wambeti Ann Ireri, Ndemo Paul Maina ambaye amekuwa naibu msajili na amekuwa akishikilia nafasi hii kwa muda, Kendagor Caroline Jepyegen na Kandet Kennedy Lenkamai. Amadi alistaafu baada ya kuhudumu kwa wadhifa huu kwa miaka kumi tangu mwaka wa 2014.