Juhudi za kutafuta amani ya kudumu DRC

  • | BBC Swahili
    5,128 views
    Wenyeviti wa Jumuiya za Afrika mashariki EAC na SADC wamekutana jijini Nairobi nchini Kenya katika juhudi za kuunganisha mazungumzo ya pande mbili kuhusu amani ya DRC. Miongoni mwa waliohudhuria ni wapatanishi wakuu ambao ni marais wa zamani Uhuru Kenyatta wa Kenya, Olusegun Obasanjo wa Nigeria, Catherine Samba-Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Sahle-Work Zewde wa Ethiopia, na Mokgweetsi Masisi wa Botswana. Viongozi hao wametoa wito kwa michakato yote inayoendelea ya kutafuta amani DRC kuwiana na mchakato wa Umoja wa Afrika AU. Je, hii ndio suluhu ya kumaliza vita ambavyo vimeendelea kwa takriban miongo mitatu DRC? Ungana na @martha_saranga saa tatu kamili katika dira ya dunia tv na pia usisahau kutembelea ukurasa wetu wa youtube wa BBCSWAHILI. #bbcswahili #kenya #drc Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw