Kaka katili Eastleigh

  • | Citizen TV
    5,067 views

    Familia moja katika mtaa wa eastleigh inataka haki baada ya binti yao kushambuliwa kikatili na kaka yake. Abdiaziz Abdullahi Daqare anadaiwa kumshambulia vikali dada yake mwenye umri wa miaka 23, Ridwan Abdullahi daqare, nyumbani kwao Eastleigh kwa madai kuwa alikuwa akimwadhibu. Kulingana na familia, shambulio hilo lilitokana na kutoridhika kwa Abdiaziz kuhusu safari ya Ridwan kwenda Uganda kumtembelea rafiki yake.