Kalonzo Musyoka adai serikali ilihusika kwenye vurugu Limuru

  • | Citizen TV
    2,245 views

    Kiongozi wa wiper Kalonzo Musyoka ameilaumu serikali kwa machafuko yaliyoshuhudia kwenye mazishi mjini Limuru hivi majuzi. Kalonzo anadai kuwa yaliyotokea Limuru yanadhihirisha wazi njama ya serikali ya kuendelea kumlenga Rigathi Gachagua na viongozi wanaoumuunga mkono. Aidha, amekosoa kutekwa nyara kwa mbunge wa zamani wa Limuru Peter Mwathi huku Mwathi mwenyewe akisimulia yalimsibu mikononi mwa waliokuwa wamemzuilia.