KALRO yaendeleza kilimo cha nyasi Naivasha

  • | Citizen TV
    221 views

    Katika juhudi za kukabiliana na uhaba wa lishe kwa mifugo, Shirika la Utafiti wa Kilimo na Mifugo –KALRO – limeanzisha mradi wa kipekee wa kilimo cha nyasi ya aina ya Lucern huko Naivasha, Kaunti ya Nakuru. Hatua hiyo inalenga kuimarisha ubora wa lishe ya mifugo ili kuwawezesha wakulima kupata maziwa zaidi , kando na kulihakikishia taifa utoshelevu wa chakula cha mifugo.