Kamati ya bunge yalalamikia kuchelewa kwa fedha za NG-CDF

  • | Citizen TV
    368 views

    Kamati ya bunge kuhusu Hazina ya Maendeleo ya Maeneo Bunge imeikashifu serikali kuhusu kucheleweshwa kwa utoaji wa fedha za CDF kwa maeneo bunge. Kamati hiyo iliyozuru eneo bunge la Awendo kukagua miradi inayofadhiliwa na NG-CDF imesema miradi kadhaa iliyopangwa mwaka huu wa fedha haijakamilika kwa sababu ya serikali kuu kuchelewesha pesa hizo.Mwenyekiti wa kamati hiyo Musa Sirma amesema wabunge wametimiza asilimia 30 hadi 40 pekee ya miradi yao iliyopangwa katika mwaka wa fedha wa 2022/2023.