Kamati ya fedha ya bunge la kitaifa yapanga kuanzisha marekebisho ya sheria

  • | K24 Video
    46 views

    Kamati ya fedha ya bunge la kitaifa inayoongozwa na mbunge wa molo kuria kimani inalenga kuanzisha mchakato wa kufanyia marekebisho sheria ya forodha ya Afrika mashariki ili kuongeza kiwango cha thamani ya mizigo ambayo wasafiri wanaowasili humu nchini wanaruhusiwa kubeba kutoka dola za marekani 500. Hatua hiyo inalenga kupunguza visa vya wakenya kulazimika kulipia ushuru bidhaa za matumizi yao wenyewe sawa na wale wanaoleta bidhaa nchini kwa lengo la biashara. Nayo mamlaka ya kra inapanga kubadili jinsi maafisa wake wanavyofuatilia ushuru katika vituo vya forodha ili kusitisha visa vya wasafiri kudhulumiwa