- 120 viewsDuration: 1:22Kamati ya utekelezaji wa ripoti ya Nadco imeandaa vikao na wakazi wa kaunti ya Taita Taveta ili kupokea maoni yao. Mwenyekiti wa kamati hiyo Daktari Agnes Zani akisema wakazi wanataka waathriwa wa maandamano ya Gen Z kulipwa fidia kwa wakati pamoja na serikali kukabili donda sugu la ufisadi. Kadhalika, kamati hiyo pia ilipokea malalamiko ya wakazi wa kaunti ya Taita Taveta wanaosema hawanufaiki na raslimali za madini na mapato ya mbuga ya Tsavo.