Kamati ya seneti yachunguza kashfa ya mafuta ya kupika

  • | Citizen TV
    911 views

    Kamati ya bunge la seneti kuhusu biashara na viwanda imeamuru mkurugenzi wa kampuni ya Charma Holdings Ruth Kinyanjui kuwasilisha kandarasi rasmi ya uagizaji wa mafuta ya kupikia kutoka kwa taasisi ya KNTC, huku uchunguzi dhidi ya madai ya kashfa ya bilioni 16 kuhusu uagizaji wa mafuta hayo ukiendelezwa. Aidha, imebainika kwamba hakujulikani penye baadhi ya mafuta hayo ya kupika yalipo licha ya kuwa yalifaa kuwasili nchini na kusambazwa kwenye maduka mbali mbali.