Kampuni za kusaga suakri Busia zalaumiwa kuibiana miwa ya wakulima

  • | West TV
    37 views
    Wakulima wa miwa katika kaunti ya busia wametakiwa kuzingatia kwa kina mikataba wanayoweka na kampuni za kusaga miwa, wakishauriwa Kuingia kwenye mikataba na kampuni itakayowekeza na hatimaye kuvuna miwa yao inapokomaa. Haya yanajiri huku kukizuka mvutano kati ya viwanda viwili vya kusaga miwa katika kaunti ya busia vinavyolaumiana kwa wizi wa miwa mashambani kinyume cha mikataba kati ya wakulima na viwanda hivyo